WS14 – WorldSports14

ZLATAN AKIRI HAELEWI HATA YEYE ANATAKA NINI

Nyota wa AC Milan ya Italia Zlatan Ibrahimovic raia wa Sweden ameacha maswali mengi kupitia gazeti la Marca kufuatia kukiria kuwa hata yeye hajui hatma yake anataka nini.

Zlatan ,38, ambaye mwaka huu Oktoba atatimiza miaka 39 ameshindwa kukiri kuwa hatma yake itakuwaje katika soka atastaafu au kuendelea kukipiga.

”Sijui hata nataka nini vitu vipya vinatokea kila siku, nani anaweza kutabiri sasa yajayo na hii corona? Tunachotakiwa ni kujaribu kuishi na kufurahia maisha”

Nyota huyo mwenye heshima kunwa nchini kwao Sweden aliwasili AC Milan ya Italia Januari 2020 katika kipindi cha dirisha dogo akipewa mkataba wa miezi sita unaomalizika Juni 30 ila mlipuko wa virusi vya corona unadaiwa kuwa AC Milan hata kama watavutiwa kuendelea nae ila hawatakuwa na pesa za kumsajili.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More