WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • WEZI WAMVAMIA CHRIS SMALLING NYUMBANI KWAKE ITALIA

WEZI WAMVAMIA CHRIS SMALLING NYUMBANI KWAKE ITALIA

Beki wa klabu ya AS Roma Chris Smalling amevamiwa nyumbani kwake akiwa na mkewe na mtoto wake wa kiume usiku wa kuamkia leo huko katika mji wa Roma nchini Italia.

Gazeti la Italia Gazzetta dello Sport limeripoti wezi hao watatu wakiwa na silaha walivunja na kuingia ndani ya nyumba ya mchezaji huyo na kumlazimisha kufungua ‘safe’ yake, na kuchukua vito vya thamani na vitu vingine.

Baada ya tukio hilo mke wa Smalling, Sam amesema waliwapigia Polisi ambapi walifika nyumbani hapo saa 11 Alfajiri, na sasa wanaendelea na uchunguzi.

Smalling aliyetua moja kwa moja AS Roma akitokea Man United mwaka jana, hakucheza mechi ya jana dhidi ya Ajax kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu ya goti.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More