WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • WACHEZA SABA UWANJANI HUKU KIPA AKICHEZA BEKI WA KATI

WACHEZA SABA UWANJANI HUKU KIPA AKICHEZA BEKI WA KATI

3-2-1 ndio mfumo walioutumia wakiwa na mpira, na walitumia 4-2-0 walipopoteza mpira.
Mmmmmh ni timu gani hiyo?

Timu ya Rionegro Aguilas ya nchini Colombia jana ililazimika kucheza mechi yao ya ligi kuu nchini humo dhidi Boyaca Chico na wachezaji saba tu kutokana na wachezaji wao 22 kuwa nje kwa sababu ya kuwa na virusi vya Corona na wengine wakiwa majeruhi.

Licha ya kuomba mechi hiyo kuahirishwa, lakini uongozi wa ligi kuu ya Colombia walikataa na hivyo timu hiyo kulazimika kucheza na wachezaji 7 huku kipa wao wa akiba Juan Valencia akicheza nafasi ya beki wa kati.

Wachezaji wao 16 walikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona na wengine walikuwa ni majeruhi.

Rionegro Aguilas wakiwa nyumbani waliweza kucheza bila kuruhusu goli kwa dakika 57.
Baada ya hapo wakaruhusu kufungwa goli 3 kabla ya mechi kumalizwa dakika ya 79 na mwamuzi Carlos Ortega na ushindi kwenda kwa Boyaca Chico.

Mechi hiyo ililazimika kumalizwa dakika ya 79 baada ya mchezaji wa Rionegro Aguilas Giovanny Martinez kuumia, na hivyo timu hiyo kubaki sita uwanjani, ambayo namba hiyo ya wachezaji haitoshi kwa mechi kuchezwa.

Baada ya mechi Aguilas waliandika katika ukurasa wao wa Twitter : “Tumepoteza mchezo, lakini tunaenda kushinda vita dhidi ya Covid-19….”

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More