WS14 – WorldSports14

VINCE CARTER ASTAAFU NBA BAADA YA MIAKA 22

Baada ya miaka 22, mchezaji wa zamani wa klabu za Raptors,Kings,na Atlanta Hawks Vince Carter leo ametangaza kustaafu kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 43

Carter awali alitangaza kustaafu mwaka jana,aliposaini mkataba wa mwaka mmoja na Atalanta Hawks, ikiwa na maana ya kuwa msimu wa 2019/20 ndio msimu wake wa mwisho.

Hata hivyo Carter hakuweka wazi kuhusu mustakabali wake wa kucheza tangu ligi ya NBA isimame Machi 11 kwa sababu ya virusi vya Corona.

Mapema mwezi huu NBA ilitangaza kuwa msimu utarejea mwezi Julai na timu 22 katika kijiji cha Walt Disney World. Hawks hawatakuwepo miongoni mwa hizo timu zitakazorejea kwa sababu ya rekodi mbovu waliyonayo msimu huu (20-47), hivyo ikimaanisha kuwa msimu wa Carter ulimalizika mwezi Machi.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More