WS14 – WorldSports14

VIATU VYA MICHAEL JORDAN VYAVUNJA REKODI YA MAUZO

Jozi za viatu zilizovaliwa na gwiji wa mchezo wa mpira wa kikapu Michael Jordan katika msimu wake wa kwanza wa NBA zimeuzwa kwa Dola za Kimarekani 560,000 (Tsh Bilioni 1.2) katika mnada wa mtandaoni uliofanyika jana Jumapili na kampuni ya mnada ya Sotheby

Viatu hivyo ambavyo vilivyobuniwa kwa ajili ya Michael Jordan mwaka 1985, vikiwa na saini yake, vilitarajiwa kuuzwa katika mnada huo kati ya dola 100,000 mpaka 150,000—lakini matarajio yamekuja vinginevyo na kuweka rekodi mpya mauzo katika kampuni hiyo ya mnada ya Sotheby.

Kama vilivyo viatu vingi vya Jordan vya Baskeball, na hivyo vilivyouzwa vilikuwa havifanana kwa ukubwa, cha kushoto kikiwa na ukubwa wa 13 na cha kulia kikiwa na ukubwa wa 13.5.
Viatu hivyo huwa na ukubwa tofauti kwa sababu mguu wa kushoto wa Jordan ni mdogo kulinganisha na mguu wake wa kulia.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More