WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • VIATU VYA MESSI KUPIGWA MNADA NA PESA KUSAIDIA WATOTO

VIATU VYA MESSI KUPIGWA MNADA NA PESA KUSAIDIA WATOTO

Viatu alivyovaa Lionel Messi alipofunga goli la kuweka rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli mengi katika klabu moja,vinauzwa na pesa itakayopatikana itaenda kusaidia watoto wanaosumbuliwa na magonjwa.

Mnada huo utafanyika kati ya April 19 na April 30 na pesa itakayopatikana itapelekwa katika Hospitali ya Vall d’Hebron University mjini Barcelona kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Messi alifunga goli hilo Disemba 22,2020 kwenye mechi dhidi ya Real Valladoid na kufikisha magoli 644, na kuvunja rekodi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Pele aliyofunga magoli 643.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More