WS14 – WorldSports14

TOTTENHAM YAKATA STAFF WAKE 20% YA MSHAHARA

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham ya England Daniel Levy ametangaza kukata mishara ya wafanyakazi wa Tottenham kwa asilimia 20 katika kipindi cha mwezi April na Mei.

Levy ametangaza makato hayo kwa staff wa Tottenham 550 nusu saa baada ya kuwapa taarifa rasmi huku akieleza kuwa makato ya wachezaji wanafikiria namna ya kufanya kutokana na klabu yao imesitisha uzalishaji kwa sasa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Maamuzi hayo ameeleza kuyachukua huku akitaka baadhi ya wafanyakazi wachukue likizo zao za mwaka kwa sababu kunusuru ajira zao za muda mrefu.

Hata hivyo uamuzi wa Levy ambaye bado hajatangaza kama atawakata wachezaji umejiwa juu na baadhi ya watu England wakihoji kwa nini anayepokea mishahara wa pauni 30,000 kwa mwaka kakatwa mshahara wakati anayepokea pauni 100,000 (mchezaji) kwa wiki hajakatwa ina maana anapokea mshahara wake wote kwa asilimia 100.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More