WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • THIERRY HENRY ATUMA SALAMU ZA SHUKURANI KWA CANTWELL

THIERRY HENRY ATUMA SALAMU ZA SHUKURANI KWA CANTWELL

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Heny ametuma salamu za shukurani kwa kiungo wa Norwich City Toddy Cantwell ambaye alionesha kuunga mkono harakati za kupambana kutetea haki za watu weusi.

Cantwell alionesha ishara ya kuunga mkono kwa kupiga goti na kunyosha mkono mmoja juu baada ya kufunga goli kwenye mchezo wa robo fainali FA Cup dhidi ya Man United juzi Jumamosi.

Kitendo hicho alichofanya ni ishara inayotumika katika kampeni ya “Black Lives Matter” inayoendelea duniani.

Thierry Henry ambaye kwa sasa ni kocha wa Montreal Impact ya MLS,aliweka picha hiyo ya Cantwell kwenye ukurasa wake wa Twitter, ikiambatana na ujumbe usemao : “ Matendo yanaongea zaidi ya maneno”. Heshima kubwa Cantwell. Ahsante kwa kusikia maumivu yetu”

Cantwell akajibu ujumbe huo kwa kushema , “Ni Mapenzi”.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More