WS14 – WorldSports14

STEPH CURRY ARUDI TENA KUANDAMANA MAREKANI

Baada ya Jumatano iliyopita kuungana na mamia ya watu huko Oakland,California katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi, nyota wa Golden State Warriors Steph Curry jana tena ameungana na kundi la waandamanaji huko Palo Alto,California katika muendelezo wa maandamano ya kupiga ubaguzi wa rangi.

Steph Curry alionekana kuongoza wimbo wa maandamano uliokuwa ukisema “Hands up – Don’t shoot” , wakimaanisha kuwa askari wasiwapige risasi.

Video nyingine ilimuonesha nyota huyo wa NBA yeye pamoja na waandamanaji wenzake wakiimba “Hey Hey,Ho Ho Donald Trump has got to go” wakiwa na maana ya kumtaka Rais wa Marekani Donald Trump inabidi aondoke madarakani.

Maandamano hayo yamekuja baada ya Polisi kumuua Mmarekani mweusi George Floyd Mei 25 huko Minneapolis,Marekani kwa kumkandamiza shingoni na kupelekea mtu huyo kukosa pumzi na kufariki.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More