WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Basketball
  • STEPH CURRY AINGIA KATIKA MAANDAMANO YA UBAGUZI WA RANGI

STEPH CURRY AINGIA KATIKA MAANDAMANO YA UBAGUZI WA RANGI

Nyota wa Warriors Steph Curry na mkewe Ayesha Curry na wachezaji wenzake wa timu yake Klay Thompson, Juan Toscano-Anderson na Damion Lee waliungana na mamia ya watu huko Oakland jana Jumatano katika maandamano ya ubaguzi wa rangi na kutafuta haki kwa George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuwawa katika mikono ya polisi huko Minneapolis wiki iliyopita.

Maandamano hayo yanafanyika katika majimbo yote 50 nchini Marekani kwa lengo na kupinga ubaguzi wa rangi na mauaji ambayo Polisi wa Marekani wamekuwa wakiyafanya.

Wanamichezo mbalimbali wamekuwa wakionesha kuunga mkono harakati hizo, wakitumia mitandao yao ya kijamii kupinga ubaguzi na kukemea mauaji hayo.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More