WS14 – WorldSports14

SIMBA SC MABINGWA MARA YA 3 MFULULIZO

Pointi 79 katika mechi 32 walizocheza, zinawafanya kuwa Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2019/20. Si wengine ni klabu ya Simba kutoka katika jiji la Dar es salaam.

Simba SC leo imefanikiwa kutangaza ubingwa huo baada ya kupata sare kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya timu ya Tanzania Prisons.

Hii ni mara ya tatu mfululizo timu ya mtaa wa Msimbazi,Kariakoo inafanikiwa kuchukua Ubingwa huo.Na katika historia huu ni Ubingwa wao wa 21 wa ligi kuu

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More