WS14 – WorldSports14

SABABU YA ETOILE DU SAHEL KUFUNGIWA USAJILI

Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Ijumaa iliyopita imepokea barua kutoka shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) likieleza kuwafungia kufanya usajili katika kipindi cha madirisha matatu ya usajili kufuatia kutolipa pesa za usajili za mchezaji Darwin Gonzales.

Gonzales ,25, raia wa Venezuela anadai kiasi cha dola 200,000 (Tsh Milioni 462.8) alipojiunga na Etoile Du Sahel Januari akitokea La Gueira kwa mkataba wa miaka mitatu ila msemaji wa Etoile Du Sahel amesema watamlipa mchezaji huyo ili kumaliza tatizo.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More