WS14 – WorldSports14

ROY KEANE AMKATAA DE GEA MAN UNITED

Mchezaji wa zamani wa Man United Roy Keane amesema timu hiyo kama inataka kuwania ubingwa wa ligi, inatakiwa kuachana na kipa David de Gea na kusajili kipa mwingine mzuri, kwani Mhispania huyo anawagharimu kwa kufanya makosa mengi makubwa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 29, amekuwa na makosa mengi makubwa msimu huu na kuleta wasiwasi wa kutetea nafasi yake ya kikosi cha kwanza.

Licha ya De Gea kupata Clean Sheet ya 13 msimu huu wa ligi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester City juzi Jumapili, Keane aliibuka tena na kutoa maneno yake dhidi ya De Gea.

“Sijawahi kuwa shabiki wake.Anafanya makosa mengi sana, makosa makubwa yanayoigharimu United pointi muhimu.”

“Tunaongelea usajili, ni sehemu ngumu ya mchezo. Hayo ni maoni yangu. Kama Manchester United wanataka kuwania ubingwa wa ligi, wanahitaji kipa mzuri” alisema Keane kupitia sky sports

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More