WS14 – WorldSports14

RONALDO DE LIMA AWAOMBA MSAMAHA WAMAMA

Ukiachana na Brazil kuibuka mabingwa wa michuano ya Kombe la Dunia 2002, kitu kingine kikubwa ambacho hukumbukwa ni aina ya unyoaji aliokuja nao mshambuliaji wa Brazil Ronaldo De Lima mwishoni mwa michuano hiyo.

Ikiwa imepita miongo karibia miwili, De Lima ameibuka na kuwaomba msamaha Wamama wote duniani ambao watoto wao waliiga aina hiyo ya kunyoa.

Pia De Lima amefichua sababu ya kwa nini alinyoa hivyo.
De Lima akinukuliwa na Sports Illustrated anasema alipata majeraha ya mguu kabla ya mechi ya nusu fainali dhidi ya Uturuki, hivyo akaamua kuja na staili hiyo ya unyoaji ili waandishi wa habari wazungumzie staili hiyo badala ya majeraha yake.
Na kweli alifanikiwa kwani vyombo vya habari viliongelea staili yake ya kunyoa tu na kusahau majeraha aliyokuwa nayo.

Katika mechi hiyo na Uturuki akafunga goli pekee na kuipeleka Brazil fainali ambapo wakashinda 2-0 dhidi ya Ujerumani, magoli yote akifunga De Lima kipindi cha pili.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More