WS14 – WorldSports14

RAIS WA CAF AONGELEA HATIMA YAKE

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad amesema bado hajaamua kama atagombea tena muhula mwingine wa Urais wa CAF

“Bado ninapokea ushauri kutoka sehemu mbalimbali za soka Afrika, nitakapokamilisha nitasema kama nitagombea au sitagombea, sifanyi hivi kwa sababu ya matakwa yangu binafsi “ Rais huyo aliiambia BBC.

Uchaguzi wa kiti hicho cha Urais utafanyika Machi 2021, miaka minne tangu Ahmad Ahmad achukue madaraka kutoka kwa Issa Hayatou

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More