WS14 – WorldSports14

NI YEYE TENA MFALME WA MELBOURNE PARK

Vitu viwili vya kuzingatia kabla ya kucheza na Novak Djokovic, hasa katika fainali za Grand Slams.
Cha kwanza ni kuwa vizuri kimwili, na cha pili kuwa vizuri kiakili.
Katika hivyo, ukikosea kimoja umekwenda na maji.
Na ndicho kilichotokea kwa Mrusi Daniil Medvedev leo katika fainali ya Australian Open 2021.
Medvedev kuanzia seti ya pili, alionesha ku-panick, akifanya makosa (unforced errors) ambayo yalimpoteza kabisa mchezoni.

Seti tatu tu zilitosha kwa Novak Djokovic kushinda fainali hiyo , akishinda 7-5,6-2,6-2 na kufanikiwa kuchukua ubingwa Australian Open kwa mara ya tatu mfululizo.

Djokovic ndiye mchezaji alishinda mara nyingi (9) ubingwa wa Australian Open,wanaomfatia ni Roy Emerson (6) na Roger Federer (6).

Novak Djokovic ambaye ndiye mchezaji namba moja kwa ubora wa tenesi Duniani kwa upande wa Wanaume, sasa amechukua Grand Slam 18 katika maisha yake, akibakiza mbili kuwafikia Roger Federer na Rafa Nadal.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More