WS14 – WorldSports14

NBA KUREJEA JULAI 31 MWAKA HUU

Ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA inataraji kurejea kuanzia Julai 31 ili kumalizia msimu ambao ulisimama tangu Machi 11 kwa sababu ya virusi vya Corona.

Mechi hizo za kumalizia msimu mpaka fainali zitachezwa Disney World Resort huko Florida Marekani ili kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Jumla ya timu 22 ndio zitakwenda kumalizia msimu, ambapo ni timu 13 kutoka ukanda wa Magharibi na timu 9 kutoka ukanda wa Mashariki ambapo kila timu itacheza mechi 8 ili kutafuta nafasi ya kucheza mtoano.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More