WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Tennis
  • Naomi Osaka ambwaga Serena Williams katika US Open

Naomi Osaka ambwaga Serena Williams katika US Open

Haitakiwi kufanya makosa pale unapopata nafasi kama hii. Pengine hayo ndio maneno ambayo Naomi Osaka aliambiwa na mama yake, Tamaki Osaka kabla ya mechi hii.

 

Naomi amekutana na Idol wake Serena Williams katika fainali ya US Open 2018 na kushinda kwa seti 6-2, 6-4.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa Naomi kuingia fainali ya Grand Slam, na hafanyi makosa ya Jurgen Klopp, anamfunga Idol wake ambaye alikuwa akitaka kuchukua kombe hili na pengine kumpa zawadi mwanae Olympia ambaye ametimiza mwaka mmoja hivi karibuni

Naomi anakuwa ni Mjapani wa kwanza kuweza kushinda ubingwa wa Grand Slam.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More