WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • MOLINGA AFICHUA MUSTAKABALI WAKE YANGA,AWAPA ONYO MASHABIK

MOLINGA AFICHUA MUSTAKABALI WAKE YANGA,AWAPA ONYO MASHABIK

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga David Molinga amethibitisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

Mshambuliaji huyo kutoka Congo amekuwa akikumbana na maneno ya mashabiki wa timu hiyo, wakiona kuwa hana uwezo katika eneo lake la ushambuliaji.

Molinga alijibu kelele zao mashabiki wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Namungo kwa kufunga magoli mawili ya kusawazisha, mchezo ukiisha kwa sare ya 2-2.

“Ninaondoka baada ya kukamilika kwa msimu huu. (Yanga) wanaweza kusajili mshambuliaji bora zaidi yangu.” – aliongea David Molinga wakati akihojiwa na gazeti la Mwanaspoti.

“Mashabiki wanapaswa kuacha kuwapigia kelele wachezaji na kuwapa maneno mabaya kama walivyofanya dhidi yangu .”

“Magoli niliyofunga dhidi ya Namungo yalitosha kuwanyamazisha wale mashabiki waliokuwa wakinidhihaki. Nilishangazwa kuona wananiomba msamaha”

“Hata hivyo, ninataka kusema kuwa sina tatizo nao na nimewasamehe. Lakini maneno yaliniumiza sana, walinikosea

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More