WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Formula 1
  • MMILIKI WA RACING POINT ALALAMIKA KUHUSU TUHUMA ZA KUIGA MIUNDO YA MERCEDES

MMILIKI WA RACING POINT ALALAMIKA KUHUSU TUHUMA ZA KUIGA MIUNDO YA MERCEDES

Mmiliki wa timu ya Racing Point Lawrence Stroll ambaye pia ni baba wa dereva wa timu hiyo Lance Stroll, amelalamikia maamuzi yaliyotolewa ya kuiadhibu timu yake kutokana na tuhuma za kuiga miundo ya magari ya timu ya Mercedes.

Bilionea huyo wa Canada na mkuu wa timu yake Otmar Szafnauer wameendelea kushikilia msimamo wao wa kuwa hawakuiga miundo ya timu nyingine kama ambavyo timu pinzani zinavyodai.

Timu za Renault, McLaren, Ferrari na Williams zimekuwa mbele katika kuwasilisha malalamiko juu ya Racing Point.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More