WS14 – WorldSports14

MICHEZO KUREJEA BILA MASHABIKI HISPANIA

Meya wa jiji la Madrid nchini Hispania Jumamosi hii ya April 18 2020 ametangaza kuwa michezo mbalimbali nchini Hispania ichezwe bila uwepo wa mashabiki uwanjani angalau hadi nyakati za majira ya joto.

Meya Jose Luis Martinez-Almeida amesikika akifanya mahojiano na radio ya Onda Cero na kueleza kuwa virusi vya corona kwa namna vilivyo sio rahisi kuvidhibiti kwa kiasi kikubwa kama utarudisha ghafla michezo katika utaratibu wake wa kawaida ikiwemo umati wa watu kuruhusiwa kuingia uwanjani.

“Katika nyakati za spring na majira ya joto hakutakuwa na shughuli yoyote itakayohudhuriwa na umati wa watu uwanjani Hispania, kwa sababu ni wazi hali (corona) haitakuwa imedhibitiwa kabisa kabisa, tutatakiwa kubadilisha tabia na mazoea yetu hata tutakaporuhusiwa kuingia mitaani” alisema Jose Luis Martinez-Almeida

 

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More