WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • MDOGO WAKE SERGE AURIER AULIWA KWA KUPIGWA RISASI

MDOGO WAKE SERGE AURIER AULIWA KWA KUPIGWA RISASI

Mdogo wa beki wa Tottenham Serge Aurier, Christopher Aurier(26) amefariki dunia kwa kupigwa risasi tumboni leo saa 11 Alfajiri nje ya Klabu za usiku huko Toulouse,Ufaransa na muuaji kukimbia.

Baada ya kupigwa risasi Aurier aliwahishwa hospitali lakini ikatangazwa kuwa ameshafariki.

Polisi walipigiwa simu mara baada ya tukio hilo kutokea na walivyofika wakalizungushia eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.

Klabu ya Tottenham leo kupitia akaunti yao ya Twitter imethibitisha taarifa hiyo ya kifo na kutoa pole kwa beki wao Serge Aurier na familia yake.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More