WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Boxing
  • MAYWEATHER KUGHARAMIA MAZISHI YA GEORGE FLOYD

MAYWEATHER KUGHARAMIA MAZISHI YA GEORGE FLOYD

Bondia mstaafu wa Marekani Floyd Mayweather ametoa ofa ya kusimamia gharama za mazishi ya George Floyd aliyeuliwa na Polisi huko Minneapolis wiki iliyopita na vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa familia ya marehemu imekubali.

Mazishi ya Floyd yanataraji kufanyika Juni 9 katika mji wa nyumbani kwao Houston,Texas.

Floyd amefariki akiwa na umri wa miaka 46 baada ya Afisa wa Polisi kumkandamiza shingoni kwa muda mrefu na kukosa pumzi na hivyo kupelekea mauti kumfika

Mauaji hayo yamepelekea kuzuka kwa maandamano nchini Marekani, ambapo watu wameingia barabarani na kwenda kwenye vituo vya polisi kushinikiza adhabu zitolewe kwa Maafisa Polisi wote waliohusika kwenye tukio hilo.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More