WS14 – WorldSports14

MAFUNZO YA BASKETBALL YA ZYBA YAZIDI KUPAMBA MOTO

Mafunzo ya Mpira wa Kikapu yanayojulikana kama(Learn basketball skills with zyba)yaliozinduliwa rasmi tarehe 8/8/2020 visiwani Zanzibar,bado yanaendelea kwa kila Jumamosi hadi itakapotimia miezi miwili.

Mafunzo haya yanawahusisha Vijana wenye umri wa miaka(15) hadi miaka (25) kwa jinsia zote.

Moja ya malengo ya Taasisi ya Zanzibar Young Basketballers Association (ZYBA) kuandaa mafunzo hayo ni kuwasaidia Vijana kukuza na kuendeleza Vipaji vyao.

Mafunzo ya tarehe 5/9/2020 yalimalizika salama na sasa wanajiandaa tena na mafunzo ya tarehe 12/9/2020 katika kiwanja cha Urafiki Primary School.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More