WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Formula 1
  • MADEREVA 14 WAPIGA GOTI,6 WASIMAMA NA KUTOA SABABU ZAO

MADEREVA 14 WAPIGA GOTI,6 WASIMAMA NA KUTOA SABABU ZAO

Madereva 14 walipiga goti moja chini kwenye ufunguzi wa msimu wa Formular 1 leo katika Austrian Grand Prix ikiwa ni ishara ya kuunga mkono mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Ni madereva sita tu ambao hawakufanya ishara hiyo ya kupiga goti, lakini baadhi yao wakieleza kuwa wanaunga mkono mapambano hayo kama wengine na kutofanya ishara hiyo haimaanishi hawapo pamoja na madereva wenzao kwenye vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Madereva hao waliosema hivyo ni Charles Leclerc wa Ferrari na Max Verstappen wa Red Bull.

Madereva wengine ambao hawakupiga goti ni Antonio Giovinazzi, Daniila Kvyat, Carlos Sainz na Kimo Raikkonnen.

Madereva wote walivaa T-shirt nyeusi za kufanana zikiwa na maandishi yakisomeka “End Racism” — maana yake “Maliza ubaguzi wa rangi”

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Lewis Hamilton yeye alivaa T-Shirt nyeusi iliyoandikwa “Black Lives Matter”

Charles Leclerc alisema kuwa hatapiga goti lakini haimaanishi kuwa hayupo pamoja na wengine kwenye mapambano hayo.
“Ninaamini kuwa kile cha muhimu ni ukweli na tabia katika maisha yetu ya kila siku kuliko (kuweka hiyo ishara) ambayo inaweza kuonekana kama utata kwa baadhi ya nchi.” Alisema dereva huyo wa Ferrari

Kwa upande wa Max Verstappen wa Red Bull, amesema kuwa yupo katika mapambano ya kutafuta usawa na vita ya ubaguzi wa rangi, lakini anaamini kila mmoja ana haki ya kujielezea mwenyewe kwa njia inayomfaa. Na kusisitiza kutopiga goti lakini ana heshimu na kuunga mkono chaguzi za kila dereva anazofanya.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More