WS14 – WorldSports14

MABO ATAKA KOCHA WA NIGERIA AFUKUZWE

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Wanawake ya Nigeria (Super Falcons) Ismaila Mabo ,76, ameeleza kuwa kama kocha mkuu wa sasa wa timu ya taifa ya wanaume ya Nigeria (Super Eagles) Mjerumani Gernot Rohr ,66, atashindwa kutwaa taji la AFCON 2021 nchini Cameroon basi afukuzwe kazi.

Mabo akizungumza na CompleteSports amelipongeza shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF) kwa kuweka katika mkataba wa kocha huyo kuwa kama anataka aendelee kubaki anabidi ahakikishe wanatwaa AFCON 2021 na kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022. “Hadi sasa Rohr amefanya vizuri lakini nafikiri kushinda medali ya shaba katika AFCON inabidi atafakari mshahara wake mkubwa anaopokea kwa kushinda mataji, tuna vipaji vya kutawala soka Afrika”- Mabo

 

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More