WS14 – WorldSports14

LUIS SUAREZ AFICHUA SIRI

Mshambuliaji Luis Suarez amefichua kitu kilichomkera zaidi kuhusu kuondoka kwake Barcelona na kwenda Atletico Madrid katika majira ya kiangazi mwaka jana. 


Suarez amesema aliambiwa na uongozi wa Barcelona amekuwa ni mzee na hivyo asingeweza kucheza kwa kiwango cha juu katika timu kubwa. 

Mshambuliaji huyo akiongea katika mahojiano na jarida la France Football, anasema aliumizwa na maneno hayo na ndipo akaamua kujiunga na Atletico Madrid ili kuwaonesha kuwa bado ana-uwezo 


Luis Suarez sasa yupo sawa na Lionel Messi katika wachezaji wanaoongoza kwa kufunga magoli katika LaLiga msimu huu, kila mmoja akiwa na magoli 16, huku Atletico wakiwa kileleni mwa ligi—Pointi 8 juu ya Barca ambao wapo nafasi ya nne.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More