WS14 – WorldSports14

LEWIS HAMILTON ASHUKA MTAANI KUANDAMANA

Dereva wa Formular 1 Muingereza Lewis Hamilton jana ameungana na waandamanaji wengine huko Hyde Park,London katika maandamano ya amani ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Maandamano hayo yamekuwa yakiendelea sehemu mbalimbali duniani na yalianza tangu Polisi kumuua Mmarekani mweusi George Floy Mei 25,2020 huko Minneapolis Marekani kwa kumkandamiza shingoni na kupelekea mtu huyo kukosa pumzi na kufariki.

Wanamichezo mbalimbali wamekuwa wakiungana na watu wengine katika maandamano ya amani ya kupinga ubaguzi huo.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More