WS14 – WorldSports14

LAPORTA ASHINDA TENA URAIS BARCELONA

laporta

Juan Laporta ameshinda nafasi ya Urais wa Klabu ya Barcelona kwa mara ya pili.


Laporta,58, ambaye ahadi yake kubwa wakati wa kampeni ilikuwa ni kumbakisha Lionel Messi, ameshinda kwa 54% katika uchaguzi huo uliofanyika jana.


Katika uchaguzi huo, Victor Font ameshika nafasi ya pili, akiwa na 30% ya kura zote na Toni Freixa akishika nafasi ya tatu.


Hii ni mara ya pili Laporta anakuwa ni Rais wa timu hiyo, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2003-2010 ambapo katika kipindi hicho tulishuhudia akimuibua kocha Pep Guardiola na Lionel Messi kuibuka kama staa wa Dunia.  


Katika kipindi hicho cha kwanza cha Urais, Laporta aliwasajili nyota kama Ronaldinho Gaucho, Samuel Eto’o na timu ikashinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mara mbili, LaLiga mara nne na Copa del Rey.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More