WS14 – WorldSports14

KWA NINI PEP GUARDIOLA ANAVAA HAYA MAANDISHI?

Kwa mechi za hivi karibuni, kocha wa Man City Pep Guardiola amekuwa akionekana kwenye mechi akiwa amevaa vazi (hoodie) lenye maneno ‘Open Arms’


Open Arms ni nini?Open Arms ni shirika lisilo la kiserikali la nchini Hispania ambalo linashughulika kuwaokoa baharini wakimbizi wanaotumia bahari kuingia barani Ulaya wakitokea nchi za Afrika, wakikimbia vita,mateso na njaa. 

Shirika hilo lina boti zake ambazo hutumika kwenda katika bahari ya Mediterranean na kuwatafuta wakimbizi hao ambao huja na vyombo vya usafiri ambavyo si salama—na hivyo wao wanawasaidia kwa kuwapakia kwenye boti zao na kuwafikisha nchi kavu. 


Pep Guardiola amekuwa akiwashika mkono kwa kuwapa msaada wa kifedha na kwa kuwatangaza ili watu wengine waweze kutoa misaada yao kuwawezesha kuendelea kufanya shughuli hiyo ya uokoaji. 


Mwaka 2018 Pep alichangia kiasi cha Pauni 130,000 (Tsh Milioni 420) kwa shirika hilo kwa ajili ya kufufua moja boti za uokoaji na pia amewahi kumualika mwanzilishi wa shirika hilo Oscar Camps kuongea na wachezaji wa Man City, ambao nao walitoa misaada yao.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More