WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Formula 1
  • KWA NIN MERCEDES WAMEBADILI RANGI YA JEZI NA GARI ZAO?

KWA NIN MERCEDES WAMEBADILI RANGI YA JEZI NA GARI ZAO?

Vilabu vya ligi kuu ya England EPL vikiwa vinavaa jezi zenye logo ya ‘Black Lives Matters’ ikiwa ni kuunga mkono wao kupaza sauti dhidi ya ubaguzi wa rangi, timu ya Mercedes ya Formula 1 aliyopo dereva mwenye asili ya rangi nyeusi Lewis Hamilton imeamua kuunga mkono juhudi hizo.

Jana katika Austrian Grand Prix,Mercedes wameanza msimu wakiwa wamebadilisha rangi ya magari yao kutoka Silver hadi rangi nyeusi huku yakiongezewa na logo ya ‘end racism’.

Madereva Lewis Hamilton na Valtteri Bottas walivaa jezi nyeusi zikichukua nafasi ya zile nyeupe walizokuwa wakitumia huku kofia ya Hamilton nayo ikiwa ni nyeusi pamoja na logo ya Black Lives Matters.

Akiongelea hili dereva Lewis Hamilton alisema “Ni vyema tukaelewa umuhimu wa haya mabadiliko iwe kwa mtu binafsi ama kampuni.”

Hamilton ambaye hakusita kumshukuru kiongozi wa timu ya Mercedes Toto Wolf alisema “Binafsi nilishawahi kuwa mhanga wa ubaguzi mimi, familia yangu na hata marafiki hivyo ninadai mabadiliko haya kwa moyo kabisa.”

Kwa upande wa Toto Wolf alisema “Ubaguzi hauna nafasi katika jamii yetu, mchezo wetu na hata timu yetu. Hii ndio imani yetu hapa Mercedes, lakini kuwa na imani peke yake na kukaa kimya haitoshi.”

Toto aliongeza kuwa “Hatutaona aibu juu ya madhaifu yetu wakati huu, tutaendesha kwa rangi nyeusi msimu wote wa 2020 tukidai mabadiliko chanya kufanyiwa kazi.”

Mbio hizi zitaendelea kwa raundi ya pili kufanyika Julai 10 zikibakia nchini Austria katika mzunguko wa Red Bull Ring.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More