WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • KWA MARA YA PILI ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJICHUA HADHARANI

KWA MARA YA PILI ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJICHUA HADHARANI

Winga wa Klabu ya Angers ya Ligue 1, Farid El Melali ameripotiwa kuwa jana Jumatano alifikishwa kituo cha Polisi huko Ufaransa kwa kutuhimiwa kujichua ( Masturbation) hadharani, ikiwa ni mara ya pili mwaka huu anafikishwa Polisi kwa kosa hilo hilo

Wakili wa mchezaji huyo Sandra Chirac Kollarik amesema Farid,22, alijibu maswali yote aliyohojiwa Polisi na baadae akaomba msamaha kwa wanawake wote aliowakwaza kwa vitendo hivyo ambavyo amefanya kipindi cha Lockdown

Mwezi Mei mwaka huu winga huyo wa Algeria alifikishwa Polisi baada ya kuonekana akijichua nje ya nyumba yake huku akimtizama mwanamke ambaye alikuwa akiishi chini yake (ground floor). Aliachiwa huru baada ya kukiri kujutia kufanya kitendo hicho

Baada ya kutoka Polisi jana, sasa mchezaji huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Agosti 25 kukabiliana na mashitaka hayo ambayo yanaweza kufanya afungwe jela kwa mwaka mmoja na faini ya Pauni 13,000 (Tsh Milion 38)

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More