WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • KOCHA WA YANGA ATOA SIRI YA UBINGWA SIMBA MSIMU HUU

KOCHA WA YANGA ATOA SIRI YA UBINGWA SIMBA MSIMU HUU

Kocha wa Klabu ya Yanga Mbelgiji Luck Eymael ameipongeza timu ya Simba kwa kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu na pia kueleza sababu ya timu hiyo kuweza kuchukua Ubingwa huo.

Simba wanachukua Ubingwa huo wakiwa wamebakisha mechi sita ligi kumalizika, ikiwa ni mara yao ya tatu mfululizo kushinda ubingwa huo na pia ni mara yao ya 21 katika historia kushinda ubingwa huo.

Akizungumza na mtandao wa Goal.Com leo kocha wa Yanga Luc Eymael amesema kuwa Simba wamestahi kuchukua Ubingwa kwani ndio timu iliyokuwa na muendelezo mzuri msimu huu kwenye ligi.

“Ninataka kuwapongeza (Simba) kwa kushinda ubingwa wa ligi. Mimi ni mtu ninayependa haki kwenye mchezo (fair play).” Luc aliuambia mtandao wa Goal leo Jumatatu.

“Tofauti kati ya Simba na Yanga katika msimamo wa ligi ilikuwa kubwa sana wakati ninawasili, Ninafikiri Yanga ilikuwa namba sita kipindi ninawasili kuchukua majukumu lakini tayari tumepanda kutoka namba sita mpaka namba mbili, si mbaya lakini Simba walistahili kushinda Ubingwa kwa sababu ndio timu iliyokuwa na muendelezo mzuri zaidi kwenye ligi.”

Kocha huyo aliwasili Yanga mwezi Januari mwaka huu kuchukua nafasi ya kocha Mwinyi Zahera aliyetimuliwa kazi kufuatia timu hiyo kutoridhishwa na muendelezo wake.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More