WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • KOCHA AJIUZULU BAADA YA KUHUKUMIWA JELA SIKU CHACHE KABLA YA KUMVAA MOURINHO

KOCHA AJIUZULU BAADA YA KUHUKUMIWA JELA SIKU CHACHE KABLA YA KUMVAA MOURINHO

Kocha wa klabu Dinamo Zagreb ya nchini Croatia Zoran Mamic amejiuzulu nafasi hiyo kuelekea mechi ya marudiano Europa League dhidi ya Tottenham baada ya mahakama ya nchini humo kumhukumu miaka minne na miezi nane jela kwa kosa la ukwepaji kodi.


Kocha huyo amehukumiwa pamoja na kaka yake Zdravko Mamic ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo. Wengine waliyokutwa na hukumu hiyo ni aliyekuwa Afisa wa kodi wa Dinamo Milan Pernar na aliyekuwa Mkurugenzi wa timu hiyo  Damir Vrbanovic


Zdravko Mamic amehukumiwa miaka sita na nusu jela, Milan Pernar ni miaka mitatu na miezi miwili, huku Damir Vrbanovic akipewa kifungo cha miaka mitatu.
Wote walishitakiwa kosa la ukwepaji kodi yenye thamani ya Pauni Milioni 1.37 (Tsh Bilioni 4.4) na kunyonya kiasi cha Pauni milioni 13.12 (Tsh Bilioni 42) kutoka kwenye uhamisho wa wachezaji katika klabu ya Dinamo Zagreb.


Dinamo Zagreb kesho katika mechi hiyo ya marudiano raundi ya 16 bora watakuwa nyumbani kuwakaribisha Spurs ambao walishinda 2-0 katika mechi ya kwanza.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More