WS14 – WorldSports14

KITAMBAA CHA UNAHODHA CHAGEUKA MSAADA SERBIA

Kitambaa cha unahodha alichokitupa Cristiano Ronaldo katika mechi dhidi ya Serbia Jumamosi iliyopita, kimechukuliwa na kwenda kupigwa mnada kwa ajili ya kukusanya hela za upasuaji wa mtoto wa miezi sita anayesumbuliwa na uti wa mgongo huko nchini Serbia.

Ronaldo alikitupa kwa hasira kitambaa hicho baada ya goli alilofunga kukataliwa kufuatia waamuzi kuona kuwa mpira ulikuwa haujavuka mstari wa goli, hata hivyo baada ya mechi mwamuzi wa mchezo aliomba msamaha kwa kosa hilo.

Mfanyakazi mmoja wa uwanjani alikiokota kitambaa hicho na kukipeleka katika kikundi cha msaada (Charity Group) ambao ndio wanakifanyia msaada kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo wa kiume, Gavril Djurdjevic

Mnada huo umeanza jana Jumanne na utafanyika kwa siku , wakiwa na lengo la kufikisha euro milioni 2.5 (Tsh Billion 6.7).

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More