WS14 – WorldSports14

JEZI ZA MESSI ZATOA CHANJO YA CORONA

Umeshawahi kuijua nguvu ya mchezaji kama Lionel Messi??!!

Staa huyo wa Argentina na Barcelona amesaidia kupatikana kwa chanjo 50,000 za virusi vya Corona kwa ajili ya wachezaji wa America Kusini kuelekea michuano ya Copa America itakayofanyika nchini Argentina na Colombia Juni 1 mpaka Julai 10 mwaka huu.

Chanjo hizo zimetolewa na kampuni ya dawa ya nchini China Sinovac baada ya Lionel Messi kuipa kampuni hiyo jezi zake tatu alizozisaini.

Messi amefanya hivyo kusaidia mpango wa shirikisho la soka la Amerika Kusini CONMEBOL wa kutaka kuwapiga chanjo ya Corona wachezaji wote wa ligi kuu za wanaume na wanawake za bara hilo kabla ya michuano hiyo itakayoanza mwezi Juni.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More