WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • JE MAN CITY WATAWAPA GWARIDE LA HESHIMA LIVERPOOL?

JE MAN CITY WATAWAPA GWARIDE LA HESHIMA LIVERPOOL?

Timu ya Man City ambayo ndio inayofuata kucheza na Liverpool mechi ijayo katika ligi kuu nchini England, inataraji kuwapa Gwaride la Heshima (Guard of Honour) Mabingwa hao wapya wa ligi kuu watakapokutana kwenye uwanja wa Etihad Alhamisi Ijayo.

Kitendo hicho cha Gwaride la Heshima si lazima, lakini ni utamaduni pale timu inaposhinda Ubingwa kabla ya siku ya mwisho ya msimu.

Ni Lini utamaduni huu ulianza?
Utamaduni huu haukuanza katika zama hizi, ulianza mwaka 1955, ambapo Man United waliwapa Chelsea Gwaride la Heshima, na sasa tamaduni hiyo imesambaa katika ligi nyingine za Ulaya.

Kabla ya mechi,timu mbili zinazokutana katika mechi husika zinafanya majadiliano kuhusu Gwaride la Heshima,na kama zitafikia maridhiano, basi Gwaride la Heshima litafanyika

Si City tu ndio wanaotaraji kuwapa Gwaride la Heshima Liverpool, ni timu zote saba watakazokutana nazo kabla ya msimu kuisha—wakiwemo mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Arsenal na Chelsea.

 

Hata hivyo uongozi wa ligi kuu nchini England unasubiriwa kupitisha kufanyika kwa kitendo hicho cha Gwaride la Heshima kwa sababu ya miongozo mipya ya kujikinga na virusi vya Corona.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More