WS14 – WorldSports14

IAN WRIGHT AIKATAA FAULO YA BRUNO

Mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni mchambuzi Ian Wright amesema ile faulo waliyopewa Man United na Bruno kupiga na kufunga haikupaswa kutolewa kwani Edinson Cavani alikuwa tayari alishaanza kuondoka hata kabla ya Fabinho kumgusa.

Hata hivyo mchambuzi mwenzake Allan Shearer alikataa maoni hayo ya Ian Wright akisema kuwa mwamuzi alikuwa sahihi kutoa ile faulo lakini alimkosoa kipa wa Liverpool Alisson Becker kwa kushidwa kuzuia shuti la Bruno.

Mechi hio iliisha kwa Man United Kushinda 3-2 na kufuzu raundi ya tano ya michuano ya FA Cup.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More