WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • HAJI MANARA ATHIBITISHA SIMBA HAIJAATHIRIKA NA CORONA KIFEDHA

HAJI MANARA ATHIBITISHA SIMBA HAIJAATHIRIKA NA CORONA KIFEDHA

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya klabu ya Simba Haji Manara amefany mahojiano na Azam TV na kueleza kuwa Simba SC janga la virusi vya corona halijaiathiri Simba SC kifedha labda katika suala zima na momentun tu lakini kifedha hawajaathirika.

“Kifedha Simba hatujayumba sababu ya corona lakini tumeyumba kwa sababu ya kukosa hali ha muendelezo wa Ligi lakini niliongea na kocha msaidizi Matola amesema wametoa program maalum kwa wachezaji kuifanya wakiwa majumbani kwao”

”Kiuchumi labda kuyumba kwake ni kule kukosa viingilio vya mlangoni kutoka kwenye mechi zetu hata nyinyi Azam TV ambao mmekuwa mnarusha tumeyamiss kikubwa sisi watu wa mpira tumemiss Ligi tumemiss ile presha ya mechi yangu leo nitashinda?”

Hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inasimama Simba SC walikuwanaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na jumla alama 71 ikicheza michezo 28 na imesalia na mechi 10, huku wakifuatiwa na Azam FC wenye jumla ya mechi 28 alama 54 ni tofauti ya alama 17 dhidi ya Simba.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More