WS14 – WorldSports14

GOMEZ ATUNDIKA DARUGA KISHUJAA UJERUMANI

Mshambuliaji Mario Gomez amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 34 baada ya kuisaidia timu yake ya Stuttgart kupanda daraja kurejea katika Bundesliga.

Gomez alifunga goli pekee la Stuttgart jana katika mechi yao ya mwisho ya ligi ambayo walipoteza kwa goli 3-1 dhidi ya Darmstadt 98. Licha ya kupoteza mechi hiyo bado Stuttgart wamemaliza nafasi ya pili na kufanikiwa kupanda kurejea kwenye ligi kuu ya Ujerumani msimu kesho.

“Hii ilikuwa ni kazi yangu ya mwisho kwa VFB Stuttgart,” alisema Gomez. “Siku zote niliota kumaliza maisha yangu ya soka hapa.”

Gomez alianza maisha yake ya soka kwenye klabu hiyo ya Stuttgart ambapo alishinda ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2006/07 kabla ya kutimkia Bayern Munich alipoenda kubeba ubingwa huo mara mbili pamoja na komba la Klabu Bingwa Ulaya 2012/13.

Baada ya kuondoka Bayern Munich mwaka 2013 akacheza vilabu vya Fiorentina, Besiktas,Wolfsburg na baadae mwaka 2018 akarejea Stuttgart kumalizia soka lake.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More