WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • GHANA WAENDELEA KUMSHAWISHI SALISU KUICHEZEA TIMU YAO

GHANA WAENDELEA KUMSHAWISHI SALISU KUICHEZEA TIMU YAO

Kocha wa timu ya Taifa ya Ghana CK Akunnor ameeleza kupitia Angel FM ya Ghana kuwa chama cha soka cha Ghana (GFA) kimekuwa kikifanya jitihada sana za kumshawishi beki wa zamani wa Real Valladolid Mohammad Salisu akubali kuchezea timu ya taifa ya Ghana, lakini bado hawajafanikiwa.

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 21, ambaye yupo mbioni kujiunga na klabu ya Southampton,amekuwa na kiwango kizuri katika msimu wa LaLiga ulioisha—mpaka kupelekea kuibuka kwa tetesi za kutakwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya kama vile Man United na Atletico Madrid.

Mzaliwa huyo wa Ghana,aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa ya Ghana Novemba mwaka jana lakini alikataa wito huo na kupelekea imani kuwa mchezaji huyo anataka kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Hispania.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More