WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Boxing
  • FURY NA AJ WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUSHUKA ULINGONI PAMOJA

FURY NA AJ WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUSHUKA ULINGONI PAMOJA

Promota wa Anthony Joshua Eddie Hearn amesema bondia wake amefikia makubaliano ya dili la mapambano mawili na bondia Tyson Fury na pambano la kwanza kati yao linaweza kufanyika majira ya kiangazi mwaka 2021

Mabingwa hao wa uzito wa juu kutoka Uingereza, wamekuwa wakitafuta kushuka ulingoni pamoja kwa muda mrefu na sasa wamefikia makubaliano katika baadhi ya vipengele, kwa mujibu wa Eddie Hearn.

“Tunafanya maendeleo makubwa.” Alisema Promota wa Joshua Eddie Hearn akizungumza na kituo cha Sky Sports

“Bado yapo mengi ya kuyakabili.Tunaangalia sehemu ya pambano na tarehe”

Promota huyo amesema bado mikataba haijasainiwa kutokana na kuwa kuna mengi ya kuweka sawa katika mazungumzo ya dili hizo, lakini cha kutia matumaini ni kuwa mabondia wote wapo kwenye makubaliano.

Tyson Fury ni bingwa wa WBC ambaye hajapoteza mchezo mpaka sasa, huku mpinzani wake Anthony Joshua ambaye amewahi kupoteza mara moja dhidi ya Andy Ruiz Jr, anashikilia mikanda ya IBF, WBA na WBO.

Kabla ya wawili hao kushuka ulingoni, Fury ana mkataba wa kupigana na Deontary Wilder kwa mara ya tatu na AJ anatakiwa kupigana na Kubrat Pulev.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More