WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Tennis
  • DJOKOVIC ATOLEWA KWA KUMPIGA NA MPIRA MWAMUZI

DJOKOVIC ATOLEWA KWA KUMPIGA NA MPIRA MWAMUZI

Mcheza Tenesi namba moja kwa ubora Duniani kwa upande wa wanaume Novak Djokovic alitolewa katika michuano ya US Open 2020 jana Jumapili baada ya kumpiga kwa bahati mbaya na mpira usoni moja ya waamuzi wa mchezo.

Djokovic alikuwa nyuma 5-6 katika seti ya kwanza kwenye mechi ya raundi ya nne dhidi ya Carreni Busta, akaupiga mpira nyuma yake na mpira ukampiga mwamuzi wa kike kwenye koo,ikampelekea mwamuzi kudondoka chini.

Djokovic akamkimbilia kumuangalia mwamuzi kama yupo sawa. Mwamuzi aliweza kusimama na kutoka uwanjani.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu na waamuzi uwanjani,Djokovic alitolewa kwenye michuano na mpinzani wake Carreni Busta kutangazwa mshindi.

Baadae kupitia mtandao wa Instagram Djokovic aliomba msamaha kwa kitendo hicho, huku akisisitiza kuwa hakudhamiria.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More