WS14 – WorldSports14
  • Home
  • News
  • DJOKOVIC APATA CORONA KWENYE MICHUANO YAKE

DJOKOVIC APATA CORONA KWENYE MICHUANO YAKE

Mchezaji namba moja wa tenesi duniani Novak Djokovic pamoja na mkewe Jelena, wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, watoto wa hawajakutwa na maambukizi hayo.

Mchezaji huyo amekutwa na maambukizi hayo siku chache baada ya michuano yake ya Tenisi aliyokuwa akiindesha katika nchi za Serbia na Croatia kukatishwa kabla ya mechi ya fainali kufuatia wachezaji wawili kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Djokovic alikosolewa vikali na watu mbalimbali kwa kuendesha mashindano hayo na kuleta wachezaji kutoka nchini nyingine licha ya uwepo wa virusi vya Corona.

Djokovic ni mchezaji wanne kupata virusi hivyo kati ka wachezaji walioshiriki michuano hiyo. Wengine ni Viktor Troicki, Grigor Dimitrov na Borna  Coric

Katika michuano hiyo hakukuwepo kuachiana umbali (Social Distancing), wachezaji wengine walikuwa wakikumbatiana na kusheherekea pamoja usiku katika klabu za usiku.

Licha ya kukutwa na maambukizi, Djokovic amesema michuano hiyo ilikuwa na lengo zuri la kuleta umoja na mshikamano baina ya nchi hizo.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More