WS14 – WorldSports14

DEREVA WA FORMULA1 APONA KATIKA AJALI YA MOTO

Katika mbio za Bahrain GP siku ya leo tukio kubwa halikuwa kwa dereva Lewis Hamilton kuibuka mshindi na nafasi ya pili na tatu kuchukuliwa na madereva wa timu ya Red Bull Max Verstappen na Alex. 

Jambo kubwa katika mbio za leo ni kwa dereva wa timu ya Hass, Romain Grosjean kufanikiwa toka salama katika ajali ya moto. Grosjean alipata ajali mwanzoni kabisa wa mbio kwenye mzunguko wa kwanza baada ya gari lake kukwaruzana na lile la Daniil Kvyat wa AlphaTauri na kwenda kujigonga kwenye vizuizi na kulipuka moto. 

Gari la usalama liliwahi fika eneo la tukio punde na wasimamizi na watoa huduma ya kwanza kufanikiwa mpa usaidizi dereva huyo kutoka katika gari hilo lililokuwa likiwaka moto.

Akiwa ametoka salama dereva hiyo alichukuliwa na kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuchukuliwa na helikopta kuwahishwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akihisiwa kuvunjika mbavu na kuwa na majeraha kidogo ya moto.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More