WS14 – WorldSports14

CORONA YACHUKUA UHAI WA RAIS WA MARSEILLE

Olympique Marseille soccer team president Pape Diouf, seen during a press conference in Marseille , southern France, Thursday, Jan. 15, 2009. Marseille signed former Arsenal and Lyon striker Sylvain Wiltord on loan for six months from division rival Rennes. (AP Photo/Claude Paris)

Pape Diouf ,68, aliyewahi kuwa Rais wa klabu ya soka ya Olympique Marseille ya Ligi Kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) afariki Dunia kwa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Diouf amefariki akiwa Dakar Senegal hospitali alipokuwa anaendelea kupatiwa matibabu licha ya familia yake kuombwa apelekwe akatibiwe Ufaransa.

Alikuwa Rais wa Marseille kwa miaka mitatu (2005-2009) kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jean-Claude Dassier.

Kupata kwake nafasi katika klabu hiyo kama Rais kuliandika historia ya kuwa mtu mweusi wa kwanza kuwa Rais wa klabu ya mpira wa miguu Ulaya, katika kipindi chote cha maisha yake Diouf alikuwa ameweka maisha yake katika soka kama mwandishi wa habari na wakala wa wachezaji soka.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More