WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • BRUNO FERNANDES AFIKIA REKODI YA CRISTIANO RONALDO

BRUNO FERNANDES AFIKIA REKODI YA CRISTIANO RONALDO

Kiungo wa Man United Bruno Fernandes ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Juni Ligi kuu nchini England, ikiwa ni mara ya pili mfululizo anashinda tuzo hiyo.

Fernandes anakuwa ni mchezaji wa saba katika historia ya ligi hiyo kushinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo, alishinda mwezi Februari na ameshinda mwezi Juni ligi iliporejea baada ya mapumziko ya Corona.

Wachezaji wengine waliowahi kufanya hivyo ni Mo Salah,Jamie Vardy,Harry Kane, Cristiano Ronaldo,Dennis Bergikamp na Robbie Fowler.

Bruno Fernandes amekuwa ni mchezaji wa kwanza wa Man United kushinda mara mbili mfululizo tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Premier League tangu afanye hivyo Cristiano Ronaldo Novemba & Disemba 2006.

Wakati huo huo Bruno Fernandes ameshinda tuzo ya goli bora la Mwezi Juni katika ligi kuu nchini England kwa goli lake alilofunga dhidi ya Brighton Juni 30.

 

 

 

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More