WS14 – WorldSports14

ALONSO KUREJEA NA RENAULT MWAKANI

Bingwa mara mbili wa dunia katika mbio za formula 1, Mhispania Fernando Alonso anatarajiwa kurejea katika mbio hizo mwaka 2021

Tetesi zimedai nyota huyu atajiunga na timu ya Renault, timu aliyoshinda nayo mataji yake mawili ya dunia mwaka 2005 na 2006 kabla ya kuhamia Ferrari na McLaren.

Aliondoka formula 1 na kwenda kushiriki mbio za LeMans 24 hours alipoibuka na ushindi mwaka 2018 na 2019 hili likimfanya abakize mshindano ya Indy500 kukamilisha malengo yake ya kushinda mataji katika mashindano matatu tofauti ya mbio za magari.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More