WS14 – WorldSports14
  • Home
  • EPL
  • ALEXANDER ARNOLD AUZA VIATU VYAKE ILI KUTOA MSAADA

ALEXANDER ARNOLD AUZA VIATU VYAKE ILI KUTOA MSAADA

Beki wa klabu ya Liverpool Trent Alexandre Arnold, ameviweka katika bahati nasibu viatu vyake alivyovaa kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Everton. Viatu hivyo ambavyo ni jozi moja, vimeandikwa ‘Black Lives Matter’ , na pia vimesainiwa na mchezaji huyo.

Pesa zote zitakazopatikana katika kushindania kushinda viatu hivyo kwa njia ya bahati nasibu, zitakwenda katika Foundation ya Nelson Mandela ambayo inafanyakazi ya kupigania uhuru na usawa kwa wote

Tiketi moja katika bahati nasibu hiyo, inauzwa Pauni moja(Tsh 2,800). Kiwango cha chini cha kununua tiketi ni tiketi mbili, na hakuna kiwango cha mwisho cha juu cha kununua tiketi.

Droo ya Bahati nasibu ya kujishindia viatu hivyo itafanyika Ijumaa ya Julai 3,2020 na mshindi atapigiwa simu au kutumia barua pepe.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More