WS14 – WorldSports14

AL AHLY WAMKATAA MWAMUZI WA CAF

Klabu ya Al Ahly ya Misri imekataa mwamuzi Mgambia Bakary Gassama kuchaguliwa na CAF kuwa mwamuzi wa kati wa mechi yao ya nusu fainali Klabu Bingwa Afrika dhidi Wydad Casablanca kwa sababu mwamuzo huyo ndiye aliyechezesha mechi yao ya robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Mamelodi Sundowns.

“Gassama alichezesha mechi yetu ya marudiano ya robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns, kivipi anaweza kuchaguliwa tena? Gassama si mwamuzi pekee katika bara hili,”. — Alisema Mkurugenzi wa soka wa Al Ahly Sayed Abdelhafid

Juni 30 CAF ilitangaza kuwa mechi za nusu fainali na fainali zitachezwa mechi moja tu, na zitachezwa nchini Cameroon.

Al Ahly watacheza mechi ya nusu fainali dhidi Wydad Casablanca huku Zamalek ikicheza dhidi ya Raya Casablanca. Mechi hizo zitachezwa kuanzia mwezi Septemba.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More